32 – Muhammad bin Yahyaa al-´Ujaykiy ametukhabarisha huko Makkah: ´Abdullaah bin ´Aliy an-Naysaabuuriy ametuhadithia: ´Abdullaah bin Sa´iyd ametuhadithia, kutoka kwa Yahyaa bin Yamaan, kutoka kwa Abu Ja´far ar-Raaziy, kutoka kwa Abul-´Aaliyah, kutoka kwa Ubayy, ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake (´Azza wa Jall):

وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ ٰ

“Na pindi Mola wako alipochukua katika wana wa Aadam kutoka migongoni mwao kizazi chao… ”

”Aliwatoa kwenye uti wa mgongo wake kama vile tone la manii. Nyuso za Mitume zilikuwa kama taa.”

Kadhalika ameipokea an-Nadhwr bin ´Arabiy kutoka kwa ´Ikrimah, ambaye amesema:

”Tone la manii likamzungumzisha na likakiri utumwa.”

Masimulizi haya kutoka kwa ´Ikrimah hayatambuliki isipokuwa kwa njia hii tu. Hata hivyo hayakuthibiti.

33 – Muhammad bin Ya´quub na al-Hasan bin Yuusuf at-Twaraa-iqiy wametukhabarisha huko Misri: Ibraahiym bin Marzuuq ametuhadithia: Rawh bin Muslim ametuhadithia: Mu´tamir bin Sulaymaan ametuhadithia: Nimemsikia baba yangu akisimulia kutoka kwa ar-Rabiy´ bin Anas, kutoka kwa Abul-´Aaliyah, kutoka kwa Ubayy, ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):

وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ ٰ

“Na pindi Mola wako alipochukua katika wana wa Aadam kutoka migongoni mwao kizazi chao… ”

”Aliwakusanya, akawafanya kuwa roho, akawatia sura na akawapa uwezo wa kuzungumza. Roho ya ´Iysaa haikuwa miongoni mwa roho hizo ambazo Allaah alichukua fungamano na ahadi kutoka kwao – roho hiyo alimtumia nayo Maryam. Allaah (Jalla wa ´Azz) amesema:

فَأَرْسَلْنَا إِلَيْهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرًا سَوِيًّا قَالَتْ إِنِّي أَعُوذُ بِالرَّحْمَن مِنكَ إِن كُنتَ تَقِيًّا قَالَ إِنَّمَا أَنَا رَسُولُ رَبِّكِ لِأَهَبَ لَكِ غُلَامًا زَكِيًّا قَالَتْ أَنَّى يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ وَلَمْ أَكُ بَغِيًّا قَالَ كَذَلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ وَلِنَجْعَلَهُ آيَةً لِلنَّاسِ وَرَحْمَةً مِّنَّا وَكَانَ أَمْرًا مَّقْضِيًّا

“Tukampelekea Roho Wetu akajimithilisha kwake kama mtu timamu. Akasema: “Najinda kwa Mwingi wa rehema usinidhuru, ukiwa ni mwenye kumcha Allaah!” Akasema: “Hakika mimi ni mjumbe wa Mola wako ili nikubashirie tunu ya kijana aliyetakasika.” Akasema: “Itakuwaje niwe na kijana na hali hakunigusa mtu yeyote? Wala mimi si kahaba!” Akasema: “Itakuwa namna hiyo. Mola wako amesema: “Haya ni rahisi Kwangu na ili Tumfanye awe alama kwa watu na rehema kutoka Kwetu. Limekuwa jambo lililokwishahukumiwa!”[1]

Alipata ujauzito na ambaye alimzungumzisha, nayo ni roho ya ´Iysaa (´alayhis-Salaam).”

Muqaatil bin Hayyaan akamuuliza: ”Roho iliingia wapi?” Akasimulia kwamba  Abul-´Aaliyah, kutoka kwa Ubayy, ambaye amesema: ”Iliingia kupitia mdomo wake.”[2]

[1] 19:17-21

[2] al-Haythamiy amesema:

“Ameipokea ´Abdullaah bin Ahmad kupitia mwalimu wake Muhammad bin Ya´quub ar-Ribaaliy, ambaye alikuwa hatambuliki. Wapokezi waliosalia ni wapokezi wa Swahiyh.” (Majma´-uz-Zawaa-id (7/25))

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 61-62
  • Imechapishwa: 11/06/2026
  • Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy