Njia mbili za mwanamke kutoa zakaah ya dhahabu zake

Swali: Kuna mwanamke anamiliki dhahabu. Je, inafaa kwake kuchelewesha kutoa zakaah ya dhahabu zake mwaka mmoja baada ya kupokea kiwango chake cha mwisho?

Jibu: Sahihi ni kwamba inafaa kwake kuitanguliza na haifai kwake kuichelewesha. Kwa sababu dhahabu inapowajibika haifai kuichelewesha isipokuwa kama kuna manufaa yanayokubalika kwa mujibu wa Shari´ah. Katika hali hii hakuna manufaa yanayokubalika kwa mujibu wa Shari´ah. Kwa hiyo ni vyema kwake kutanguliza zakaah, na inafaa pia kutoa zakaah ya kila kitu  ndani ya wakati wake.

Ikiwa hajui ni wakati gani alipomiliki mali yake kwa namna ya kwamba akatilia shaka kama ilikuwa Muhrram au Swafar, basi haitowajibika kwake isipokuwa kutoa zakaah katika Swafaa.

Lakini ikiwa anajua ni wakati gani alipomiliki mali yake, basi kuna njia mbili za kutoa zakaah:

1 – Kama alimiliki dhahabu fulani katika Muharram, nyingine katika Rabiy´ al-Awwal, nyingine katika Jumaadaa al-Uulaa na nyingine katika Sha´baan, basi anaweza kutoa zakaah ya zote hizi katika Muharram. Katika hali hii anakuwa ametoa zakaah kwa kutanguliza. Na wala haijuzu kuchelewesha zakaah ya Muharram mpaka katika Sha´baan.

2 – Anaweza pia kutoa zakaah aliyomiliki kwenye kila mwezi katika mwezi wake; aliyomiliki Muharram akaitoa Muharram na kadhalika.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/304-305)
  • Imechapishwa: 11/06/2026