15. Kama wadudu wachungu kwenye mawimbi makubwa

Isitoshe wafasiri wa Qur-aan wametofautiana juu ya maana ya kizazi chao, utambuzi wao wakati alipotoa kwenye mgongo wa Aadam, akachukua lile fungamano lao la kwanza na akawashuhudisha juu ya nafsi zao: ”Je, Mimi siye Mola wenu?” Lakini wameafikiana kwamba walikuwa katika umbile la mdudu mchungu. Kisha wakatofautiana ambapo baadhi yao wakasema walikuwa roho bila viwiliwili na utambuzi bila ya akili. Wengine wakasema kuwa walikuwa ni roho na viwiliwili vyao na utambuzi kwa akili zao. Maoni ya kwanza ndio sahihi zaidi kutokana na mapokezi ya kwamba Allaah alichukua fungamano kutoka kwao pale Alipowatoa kwenye mgongo wa Aadam, kana kwamba walikuwa wadudu wachungu kwenye mawimbi makubwa ya maji. 

31 – Ibraahiym bin Muhammad ar-Ramliy ametukhabarisha: Muusa bin Haaruun ametuhadithia: Shaybaan ametuhadithia: Abu Hilaal ametuhadithia: Abu Hamzah ametuhadithia, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):

وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ ٰ

“Na pindi Mola wako alipochukua katika wana wa Aadam kutoka migongoni mwao kizazi chao.”

”Allaah alichukua fungamano la wana wa Aadam kutoka kwenye migongo yao, kutoka kwenye mawimbi makubwa ya maji, kana kwamba walikuwa wadudu wachungu kwenye mawimbi makubwa ya maji.”

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 60-61
  • Imechapishwa: 11/06/2026
  • Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy