Watu wa tafsiri wametofautiana juu ya maneno Yake (Jalla wa ´Azz):

شَهِدْنَا 

”… tumeshuhudia!”

Baadhi wamesema kuwa ushahidi huo ni kutoka kwa Allaah Mwenyewe na Malaika Wake baada ya watu kushuhudia uola wa Allaah pale Alipowaambia:

أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ 

“Je, Mimi siye Mola wenu?” Wakasema: “Ndio bila shaka… ”

Ndipo Allaah akasema na Malaika Wake wameshuhudia ushuhuda wao.

30 – Muhammad bin Ya´quub bin Yuusuf an-Naysaabuuriy na al-Hasan bin Yuusuf at-Twaraa-ifiy ametukhabarisha huko Misri: Ibraahiym bin Marzuuq ametuhadithia: Rawh bin Aslam ametuhadithia: Mu´tamar bin Sulaymaan ametuhadithia: Nimemsikia baba yangu akisilimua kutoka kwa ar-Rabiy´ bin Anas, kutoka kwa Abul-´Aaliyah, kutoka kwa Ubayy bin Ka´b, ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake (Jalla wa ´Azz):

أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَا ۛ أَن تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَـٰذَا غَافِلِينَ أَوْ تَقُولُوا إِنَّمَا أَشْرَكَ آبَاؤُنَا مِن قَبْلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةً مِّن بَعْدِهِمْ ۖ أَفَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ الْمُبْطِلُونَ

“Je, Mimi siye Mola wenu?” Wakasema: “Ndio bila shaka, tumeshuhudia ili msije kusema Siku ya Qiyaamah “hakika sisi tulikuwa tumeghafilika nayo haya au mkasema “hakika baba zetu ndio walioshirikisha kabla, nasi tulikuwa kizazi baada yao. Basi Utatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wabatilifu?”

”Aliwakusanya wote, akawafanya kuwa roho, akawatia sura na akawapa uwezo wa kuzungumza. Akachukua ahadi na fungamano kutoka kwao na akawashuhudisha juu ya nafsi zao:

أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَا ۛ أَن تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَـٰذَا غَافِلِينَ 

“Je, Mimi siye Mola wenu?” Wakasema: “Ndio bila shaka, tumeshuhudia ili msije kusema Siku ya Qiyaamah “hakika sisi tulikuwa tumeghafilika nayo haya?”

Akasema: ”Mimi nakushuhudisheni juu yenu mbingu saba na baba yenu Aadam, msije mkasema siku ya Qiyaamah kwamba hamkuyajua haya. Tambueni ya kwamba hapana mungu wa haki mwingine asiyekuwa Mimi na wala hakuna mola mwingine zaidi Yangu, hivyo msinishirikishe na chochote. Nitakutumieni Mitume ambao watakukumbusheni ahadi na fungmano Langu. Nitakuteremshieni Vitabu.” Wakasema: ”Tunashuhudi ya kwamba Wewe ndiye Mola Wetu. Hatuna mola mwingine asiyekuwa Wewe. Hatuna mungu mwingine asiyekuwa Wewe.” Siku hiyo ndio wakamkubalia kumtii.”

Wengine wakasema kwamba Aayah:

أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ 

“Je, Mimi siye Mola wenu?” Wakasema: “Ndio bila shaka… ”

ni Mitume ndio waliojibu namna hiyo. Maoni hayo yamesemwa na Wahb bin Munabbih na ´Abdul-Malik bin Abiy Yaziyd as-Swan´aaniy. Tafsiri hiyo inaafikiana na kisomo kinachosema:

أَن يَقُولُواْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ

”… ili wasije kusema Siku ya Qiyaamah… “

Hicho ni kisomo cha watu wa Makkah na Baswrah, na kisomo cha watu wengi wa Madiynah ni:

أَن تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ 

“… ili msije kusema Siku ya Qiyaamah… ”

Kwa maana kwamba wasije kusema siku ya Qiyaamah kwamba walikuwa hawajui.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 60-61
  • Imechapishwa: 11/06/2026
  • Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy