13. Kila chema kwenye mkono wa kulia wa Allaah

28 – ´Abdur-Rahmaan bin Yahyaa bin Mandah na ´Abdullaah bin Ibraahiym al-Muqriy wametukhabarisha: Abu Mas´uud ar-Raaziy ametuhadithia: Muslim bin Ibraahiym ametukhabarisha: Rawh bin al-Musayyab ametuhadithia, kutoka kwa Yaziyd al-Baswriy, kutoka kwa Ghunaym bin Qays, kutoka kwa Abu Muusa, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Wakati Allaah alipomuumba Aadam, alimshika kutoka mgongoni mwake kwa ngumi mbili; kila kizuri kikaanguka kwenye mkono Wake wa kuume na kila kibaya kikaanguka kwenye mkono Wake mwingine wa kushoto. Akasema: ”Hawa wa kulia ni watu wa Peponi, hawa wa kushoto ni watu wa Motoni –  na Sijali.” Kisha wakarudi mgongoni mwa Aadam. Wanazaana kutokana na hivo.”

29 – Ahmad bin Muhammad bin Ibraahiym, mtumwa wa Banuu Haashim aliyeachwa huru, ametukhabarisha: Abu Umayyah at-Twusiy Muhammad bin Ibraahiym ametuhadithia: Husayn bin Muhammad al-Marwaziy ametuhadithia: Jariyr bin Haazim ametuhadithia, kutoka kwa Kulthuum bin Jabr, kutoka kwa Sa´iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Allaah alichukua fungamano kutoka mgongoni mwa Aadam (´alayhis-Salaam) kwa Nu´maan, kwa maana ´Arafah, ambapo Akatoa mgongoni mwake kila kizazi alichoumba. Halafu Akawatawanya mbele yake kama mdudu chungu na akawazungumzisha:

أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَا ۛ أَن تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَـٰذَا غَافِلِينَ أَوْ تَقُولُوا إِنَّمَا أَشْرَكَ آبَاؤُنَا مِن قَبْلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةً مِّن بَعْدِهِمْ ۖ أَفَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ الْمُبْطِلُونَ

“Je, Mimi siye Mola wenu?” Wakasema: “Ndio bila shaka, tumeshuhudia ili msije kusema Siku ya Qiyaamah “hakika sisi tulikuwa tumeghafilika nayo haya au mkasema “hakika baba zetu ndio walioshirikisha kabla, nasi tulikuwa kizazi baada yao. Basi Utatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wabatilifu?”

Husayn al-Marwaziy amepwekeka katika kusimulia Hadiyth hii kutoka kwa Jariyr bin Haazim, ambaye alikuwa madhubuti. Hammaad bin Zayd, ´Abdul-Waarith, Ibn ´Ulayyah na Rabiy´ah bin Kulthuum wameisimulia kutoka kwa Kulthuum bin Jabr, kutoka kwa Sa´iyd bin Jubayr, kama masimulizi ya Ibn ´Abbaas. Vivyo hivyo ameipokea Habiyb bin Abiy Thaabit, ´Aliy bin Badhiymah na ´Atwaa’ bin as-Saa-ib, kutoka kwa Sa´iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn ´Abbaas. ´Atwaa’ amezidisha katika masimulizi yake:

”Allaah (´Azza wa Jall) alimshusha Aadam Dhuknaa na akamfuta mgongo wake.”

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 57-58
  • Imechapishwa: 11/06/2026
  • Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy