Ibn Abiyl-´Izz al-Hanafiy (Rahimahu Allaah) amesema:

”Maneno ya at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) yanaraddi ile fikira inayosema kuwa maneno ya Allaah ni maana isiyosikika, na kwamba kile kinachosikika, kinachosomwa na kinachoandikwa sio maneno ya Allaah bali ni ibara yake. at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

”Kwake ndio imeanza kwa njia ya maneno… ”

Vivyo hivyo Salaf wengine wamesema:

”Kwake ndiko imeanza na Kwake ndiko itarejea.”

Wamesema kuwa Qur-aan imeanza Kwake kwa sababu Jahmiyyah, Mu´tazilah na wengineo wanasema kuwa Allaah aliumba maneno mahali na maneno yakaanza kutokea maeneo hayo. Ndipo Salaf wakasema kuwa Qur-aan imeanza Kwake kwa maana ya kwamba Yeye ndiye wa Kwanza kuizungumza, na si kwamba imetoka kwa baadhi ya viumbe. Allaah (Ta´ala) amesema:

تَنزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ

“Ni uteremsho wa Kitabu kutoka kwa Allaah, Mwenye nguvu asiyeshindika, Mwenye hekima.”

وَلَوْ شِئْنَا لَآتَيْنَا كُلَّ نَفْسٍ هُدَاهَا وَلَـٰكِنْ حَقَّ الْقَوْلُ مِنِّي

“… lakini imethibiti kauli kutoka Kwangu… ”[1]

قُلْ نَزَّلَهُ رُوحُ الْقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ لِيُثَبِّتَ الَّذِينَ آمَنُوا وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ

“Sema: “Ameiteremsh Roho Mtakatifu kutoka kwa Mola wako kwa haki ili iwathibitishe wale walioamini na ni mwongozo na bishara njema kwa waislamu… ”[2]

Kusema kwamba Kwake ndio itarudi maana yake ni kuwa Qur-aan itanyanyuliwa kutoka vifuani na kwenye misahafu na hakuna Aayah yoyote itakayobaki katika vitu hivyo, kama yanavyoshuhudia hayo mapokezi mengi. Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:

”…. jambo ambalo halitakiwi kufanyiwa namna… ”

Bi maana namna ya maneno yake haitambuliki. Amesema:

”Sio mafumbo na Akaiteremsha kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa njia ya Wahy.”

Qur-aan sio mafumbo. Amemteremshia nayo kupitia kwa Malaika. Malaika Jibriyl akaiskia kutoka kwa Allaah, Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaisikia kutoka kwa Malaika ambapo akawasomea nayo watu. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَقُرْآنًا فَرَقْنَاهُ لِتَقْرَأَهُ عَلَى النَّاسِ عَلَىٰ مُكْثٍ وَنَزَّلْنَاهُ تَنزِيلًا

“Qur-aan Tumeigawanya sehemu mbalimbali ili uwasomee watu kwa kituo na tumeiteremsha mteremsho wa kidogo kidogo.”[3]

نَزَلَ بِهِ الرُّوحُ الْأَمِينُ عَلَىٰ قَلْبِكَ لِتَكُونَ مِنَ الْمُنذِرِينَ

“Ameiteremsha haya Roho mwaminifu – juu ya moyo wako ili uwe miongoni mwa waonyaji.”[4]

Aidha Aayah hizi zinathibitisha kuwa Allaah (Ta´ala) yuko juu.”[5]

[1] 32:13

[2] 16:102

[3] 17:106

[4] 26:193

[5] Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (1/195-196).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 27-28
  • Imechapishwa: 17/09/2024