Swali: Kufanya punyeto ni katika uzinzi wa mkono?

Jibu: Ndio kinachodhihiri, uzinzi unaweza pia kufanyika kwa usiokuwa mkono. Mtu anaweza kujichua kwa usiokuwa mkono. Kwa kufupisha ni kwamba ni aina fulani ya uzinzi wa haramu, kwa sababu ni jambo linaingia ndani ya maneno Yake (Ta´ala):

فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ

“Lakini atakayetaka kinyume ya hayo, basi hao ndio waliovuka mipaka.” (23:07)

Anaweza kutumia usiokuwa mkono. Kuna vitu vya bandia wanavyotumia. Tunamuomba Allaah usalama. Tunachotaka kusema ni kwamba ni haramu na dhambi kwa mujibu wa wanazuoni wengi. Haijuzu kwa sababu ni jambo linaingia ndani ya maneno Yake (Ta´ala):

فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ

“Lakini atakayetaka kinyume ya hayo, basi hao ndio waliovuka mipaka.”

Jengine ni kwamba ni jambo lina madhara mengi. Kunaweza kumpelekea mwenye kufanya hivo katika unyonge, udhaifu wa akili na kukosa kizazi. Baadhi ya wanazuoni wa sasa wameandika juu ya hilo na wakanukuu maneno ya madaktari juu ya madhara yake mengi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24243/هل-استعمال-العادة-السرية-من-زنا-اليد
  • Imechapishwa: 17/09/2024