14. Qur-aan – kutoka kwa Allaah kwenda kwa Jibriyl kwenda kwa Muhammad kwa Maswahabah

Shaykh Muhammad bin Maaniy´ (Rahimahu Allaah) amesema:

”Qur-aan tukufu ni maneno ya Allaah, inapokuja katika matamshi na maana yake. Ni kosa kuona kuwa Qur-aan ni matamshi peke yake pasi na maana, kama wanavosema Mu´tazilah. Kama ambavo ni kosa kuona kuwa Qur-aan ni maana pasi na matamshi, kama wanavosema Kullaabiyyah wapotevu na wengine waliowafata katika batili yao katika wanafalsafa wanaosimangwa.

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanasema na kuamini kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah na yaliyoteremshwa na hayakuumbwa. Matamshi na maana yake si kingine isipokuwa ni maneno ya Allaah. Jibriyl ameyasikia kutoka kwa Allaah, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameyasikia kutoka kwa Jibriyl na Maswahabah wameyasikia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imeandikwa kwenye misahafu, imehifadhiwa ndani ya vifua na inasomwa na ndimi. Haafidhw Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

Kadhalika Qur-aan si vyenginevyo isipokuwa ni maneno ya Allaah

yenye kusikiwa kutoka Kwake kikweli na kwa uwazi

Yote ni maneno ya Mola na si baadhi yake

Matamshi na maana yake havikuumbwa

Ni uteremsho kutoka kwa Mola wa walimwengu

inapokuja katika matamshi na maana – bila upindaji[1][2]

[1] an-Nuuniyyah (1/113).

[2] Haashiyah ´alaa al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 18-21

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 26-27
  • Imechapishwa: 17/09/2024