15. Ni ipi hukumu ya kununua magazeti ya maonyesho ya mitindo kwa ajili ya kufunika nayo na mitindo mbalimbali ya mavazi ya wanawake?

Swali 15: Ni ipi hukumu ya kununua magazeti ya maonyesho ya mitindo kwa ajili ya kufunika nayo na mitindo mbalimbali ya mavazi ya wanawake? Ni ipi hukumu ya kubaki nayo baada ya kunufaika nayo na yamejaza picha za wanawake?

Jibu: Hapana shaka kuwa kununua magazeti ambayo hayana jengine zaidi ya picha ni haramu. Kwa sababu kuhifadhi picha ni haramu kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Malaika hawaingii kwenye nyumba ilio ndani na picha.”[1]

Jengine ni kuwa wakati alipoona picha kwenye mto wa ´Aaishah, alisimama na hakuingia ndani na akaona machukizo yake usoni mwake. Magazeti haya ambayo yanaonyesha fasheni yanatakiwa kukaguliwa na si kila nguo inafaa. Pengine nguo hizi zinazonyesha sehemu za siri za mtu ima kutokana na kubana kwake au mfano wake. Pengine vilevile mavazi haya ni miongoni mwa mavazi maalum ya makafiri, na kujifananisha na makafiri ni jambo la haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”[2]

Kwa hivyo kile ninachowanasihi ndugu zangu wote wa kiislamu na khaswa wanawake wa kiislamu wajiepushe na nguo hizi kwa sababu baadhi ya nguo zinakuwa na kujifananisha na wasiokuwa waislamu na nyenginezo zinaonyesha uchi. Jengine ni kwamba wanawake kutaka kuwa na kila vazi jipya linalotoka, mara nyingi litapelekea kubadilisha desturi zetu, ambazo chimbuko lake ni dini yetu, na kwenda katika desturi nyenginezo zenye kutoka kwa wasiokuwa waislamu.

[1] al-Bukhaariy, Muslim na wengineo.

[2] Ahmad na Abu Daawuud kwa cheni ya wapokezi ilio nzuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah, uk. 24
  • Imechapishwa: 01/03/2023