15- Muheshimiwa Shaykh Dr. Jaabir at-Twayyib bin ´Aliy (Rahimahu Allaah) – Qaadhiy na muhubiri katika Msikiti Mtakatifu wa Makkah


Amesema (Rahimahu Allaah) katika dibaji yake ya kitabu “Jamaa´ah Waahidah laa Jamaa´aat”:

Hii ni dibaji ambayo huenda wengi wanaijua na kwa mnasaba wa baadhi ya wanafunzi ambao wamewafikishwa kuutumia wakati wao kuwanufaisha Ummah na kupupia katika kuwanufaisha ndugu zao kwa yale walio na haja nayo. Miongoni mwa watu hawa ambao wamewafikishwa katika haya – Allaah Akitaka – ni muheshimiwa Dr. Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy, mtunzi wa vitabu vyenye maana na Ruduud za kishujaa, ambavyo havitoki nje ya Qur-aan, Sunnah na kauli za wema waliotangulia… Kwa kukhitimisha ninasema ya kwamba Ustadhw wetu na mwanachuoni wetu mtukufu Dr. Rabiy´ amebainisha haki kwa yule anayeitafuta.”[1]

[1] Tazama dibaji ya kitabu cha Shaykh Rabiy´ ”an-Naswr al-´Aziyz”

  • Mhusika: Shaykh Khaalid bin Dhwahwiy adh-Dhwafayriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.rabee.net/ar/sharticles.php?cat=12&id=57
  • Imechapishwa: 05/12/2019