Vipi ikiwa mwezi haukutimia siku 30 kwa ambaye ana kafara ya mwezi mzima?


Swali: Kuna mtu ana kafara ya kufunga miezi miwili; Rajab na Sha´baan. Je, akamilishe miezi hii miwili au afuate kalenda?

Jibu: Ikiwa mwezi wa Rajab umethibiti kuanza kwa kuonekana na Ramadhaan imethiti kuanza kwa kuonekana ambapo Rajab ilikuwa masiku ishirini na tisa na Sha´baan ilikuwa masiku ishirini na tisa, katika siku sitini kumepungua siku mbili. Tunasema kuwa inasihi kufanya hivo. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) hakusema mtu afunge siku sitini kama  alivosema kulisha masikini sitini inapokuja katika kafara ya kumfananisha mke na mama. Bali alisema kufunga miezi miwili. Mwezi ni ule unaokuwa baina ya kuonekana miezi miwili. Ni mamoja ni siku ishirini na tisa au siku thelathini. Au mwezi wa kwanza ikawa siku ishirini na tisa na mwezi wa pili ikawa siku thelathini. Muhimu ni kwamba kile ambacho Allaah amekiwekea mpaka wa mwezi kinakuwa kwa mwezi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1383
  • Imechapishwa: 05/12/2019