Kama ambavyo kutoa jina ni haki ya baba kadhalika mtoto ananasibishwa na baba na si mama. Anaitwa kwa ubini wa baba yake na si wa mama yake. Kunasemwa “Fulani, mwana wa mwanaume fulani” na si “Fulani, mwana wa mwanamke fulani”. Pindi anapoitwa kunasemwa “Ee, mwana wa mwanaume fulani” na sio “Ee, mwana wa mwanamke fulani”. Allaah (Ta´ala) amesema:

ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِندَ اللَّـهِ

“Waiteni kwa [majina ya] baba zao, hivyo ndio uadilifu zaidi mbele ya Allaah.” (33:05)

Siku ya Qiyaamah watu wataitwa kwa majina ya baba zao. Imethibiti kupitia kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mdanganyifu atapewa bendera siku ya Qiyaamah na kutasemwa: “Huu ni udanganyifu wa fulani, mwana wa fulani.”[1]

Haya ni katika siri za Shari´ah. Kwa sababu unasibisho kwa baba unatoa utambuzi bora zaidi na upambanuzi wa wazi zaidi. Baba ndiye mwangalizi wa mtoto na mama sawa nyumbani na nje ya nyumbani. Kwa ajili hiyo ndio maana baba anaonekana misikitini na masokoni, anajiweka khatarini wakati anaposafiri ili aweze kuilisha familia na kuangalia manufaa yao. Ndio maana inamstahikia yeye zaidi mtoto akanasibishwa kwake na si mama ambaye Allaah (Ta´ala) amempa maamrisho yafuatayo:

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ

“Kaeni majumbani mwenu.” (33:33)

[1] al-Bukhaariy (1735).

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 15
  • Imechapishwa: 18/03/2017