14. Mtoto kumpa jina ni haki ya baba

Hakuna tofauti yoyote juu ya kwamba kumpa mtoto jina ni haki ya baba. Mama hana haki yoyote ya kuzozana katika suala hili. Wakizozana basi chaguo la baba ndio lenye kufanya kazi. Kujengea juu ya hili mama asigombane na wala asizozane. Hata hivyo mashauriano kati ya wazazi ni jambo zuri kwa ajili ya maradhiano, mapenzi na kukomaza uhusiano.

Imepokelewa jinsi kulikuwepo Maswahabah wengi (Radhiya Allaahu ´anhum) ambao walikuwa wakiwapeleka watoto wao wachanga kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili awape majina. Ni jambo lenye kufahamisha kuwa baba ndiye mwenye haki ya kumtaka ushauri mwanachuoni wa Sunnah, mtu mwaminifu katika Ahl-us-Sunnah, juu ya jina zuri kwa mtoto wake mzaliwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 14
  • Imechapishwa: 18/03/2017