15. Tawhiyd-ul-´Ibaadah ndio maana ya “hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah”

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mlango wa tatu

Tawhiyd-ul-´Ibaadah ndio maana ya “hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah”

Tawhiyd hii ndio maana ya maneno yako “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah”.

MAELEZO

Tawhiyd hii ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alilingania kwayo ndio maana ya “hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah”, bi maana hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah (´Azza wa Jall). Walikuwa wakijua kuwa maana yake ni hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah. Walikuwa wakitambua kuwa haina maana ya kuwa hakuna muumbaji, mwenye kuruzuku wala kuendesha mambo isipokuwa Allaah. Walikuwa wakitambua kuwa haina maana ya kuwa hakuna mwenye kuweza kuvumbua kitu kutoka katika kitu kisichokuwepo isipokuwa Allaah, kama wanavyosema wanafalsafa wengi. Hakika maana hii washirikina hawakuwa wakiipinga. Maana waliokuwa wakiipinga ilikuwa ni hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah. Amesema (Ta´ala) juu yao:

أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عُجَابٌ وَانطَلَقَ الْمَلَأُ مِنْهُمْ أَنِ امْشُوا وَاصْبِرُوا عَلَىٰ آلِهَتِكُمْ ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ يُرَادُ مَا سَمِعْنَا بِهَـٰذَا فِي الْمِلَّةِ الْآخِرَةِ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا اخْتِلَاقٌ

“Amewafanya miungu wote hawa kuwa mungu Mmoja? Hakika hili ni jambo la ajabu mno! Na wakaondoka wakuu miongoni mwao [wakisema]: “Nendeni na subirini juu ya miungu yenu, hakika hili ni jambo linalotakwa. Hatukusikia haya katika dini ya mwisho, haya si chochote isipokuwa ni jambo lilozushwa tu.”” (38:05-07)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kash-ish-Shubuhaat, uk. 26-30
  • Imechapishwa: 07/10/2023