15. Kumfananisha al-Albaaniy na at-Turaabiy

Mwandishi amemfananisha al-Albaaniy na Hasan at-Turaabiy[1] ambaye anaonelea umoja wa dini, anaona kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakulindwa na kukosea katika khabari zake za dunia, wakuu wa nchi wana haki ya kutunga sheria zao wenyewe, hukumu za Shari´ah zinatakiwa kufanywa upya kwa mujibu wa maendeleo ya mazingira yanavyopelekea na maoni yake mengine yaliyopinda yanayopelekea kufuru.

Kumfananisha al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) na at-Turaabiy ni uongo mkubwa na jinai mbaya kabisa ambayo haitakiwi kukubaliwa wala kuyanyamazia.

[1] Uk. 05

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 37
  • Imechapishwa: 24/11/2018