14. Maamuma kubeba msahafu nyuma ya imamu

Swali: Ni ipi hukumu maamuma kubeba msahafu ndani ya swalah ya Tarawiyh?

Jibu: Sijui msingi wa jambo hilo. Udhahiri ni yeye kuwa na unyenyekevu, kuwa mtulivu na asichukue msahafu. Bali aweke mkono wake wa kuume juu ya mkono wake wa kushoto, kama ilivyo Sunnah. Aweke mkono wake wa kulia juu ya kiganja chake cha kushoto kwenye kifundo na aiweke juu ya kifua. Kufanya hivi ndio maoni yenye nguvu na bora zaidi. Kubeba msahafu kutamshughulisha na Sunnah hii. Isitoshe moyo na macho yake vinaweza kumshughulisha kurejea zile kurasa, Aayah na kumsikiliza imamu. Naona kwamba kuacha mambo hayo ndio Sunnah, asikilize, anyamaze na asitumie msahafu. Kama yuko na elimu basi atamsaidia imamu. Vinginevyo atasaidiwa na watu wengine. Isitoshe tukadirie kuwa imamu amekosea na asisaidiwe halitodhuru hilo muda wa kuwa sio al-Faatihah. Kinachodhuru ni katika al-Faatihah peke yake. Kwa sababu al-Faatihah ni nguzo ya lazima. Lakini akiacha baadhi ya Aayah – mbali na al-Faatihah – halidhuru hilo ikiwa nyuma yake hakuna wa kumzindua. Kukiwepo mtu anayebeba msahafu kwa sababu ya imamu pengine jambo hilo halina neno. Lakini kusema kila mmoja anabeba msahafu ni kitu kinachoenda kinyume na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 16
  • Imechapishwa: 12/04/2022