14. Kile kilichokuwa kinamruhusu kutofunga kimeondoka wakati wa mchana

Swali: Anayekula mchana wa Ramadhaan kutokana na udhuru, kama vile safari au ugonjwa, na baadaye udhuru wake ukaondoka. Je, atatakiwa kuendelea kula na kunywa au atajizuilia?

Jibu: Analazimika kujizuilia siku yake iliyobaki kwa sababu ni miongoni mwa watu walioshuhudia mwezi. Baadaye atalipa siku hiyo kwa sababu hakufunga siku nzima. Anaingia ndani ya maneno Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi mpya na afunge na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi atimize idadi katika masiku mengine.”[1]

[1] 02:185

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 20
  • Imechapishwa: 20/03/2022