Swali: Je, inafaa kwa muislamu kutofunga akisafiri kwa ajili ya pikniki au sababu nyingine? Ni sharti zipi za safari ili ifae kula?

Jibu: Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi mpya na afunge na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi atimize idadi katika masiku mengine.”[1]

Inafaa kwa muislamu kufungua katika Ramadhaan ikiwa masafa ya safari ni sawa na ile inayomruhusu yeye kufupisha swalah. Hahitaji kufunga katika Ramadhaan ikiwa safari imeruhusiwa na si safari ya maasi. Allaah anasema:

فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi mpya na afunge na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi atimize idadi katika masiku mengine.”

[1] 02:185

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 20
  • Imechapishwa: 20/03/2022