Swali: Bwana mmoja amempoteza mwanae ambaye alikuwa hafungi Ramadhaan kutokana na sababu inayokubalika katika Shari´ah. Je, inafaa tukamfungia?

Jibu: Asifungiwe swawm ya Ramadhaan. Ikiwa sababu inatokana na kutokuweza, kwa sababu maradhi yake ni maradhi ya khatari, basi huyu atatolewa chakula kwa kila siku moja iliyompita. Bi maana 45 kg mwezi mzima. Hapa ni pale ambapo hakufunga kwa sababu maradhi yake ni sugu yasiyotarajiwa kupona; huyu atatolewa chakula akiwa bado yuko na fahamu. Hata hivyo kama alikuwa ameshapoteza fahamu kipindi alipofariki, basi hatofungiwa wala kutolewa chakula.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 20/03/2022