11. Mwanamke mfungaji imerudi damu baada ya ada yake ya mwezi

Swali: Mwanamke mfungaji ambaye imemrejelea damu yake siku mbili baada ya kutwahirika analazimika kufungua? Je, analazimika kulipa yale masiku aliyofunga?

Jibu: Ikiwa damu ya hedhi hiyo ni ile inayotambulika, basi asubiri mpaka siku kumi na tano. Ikiwa ada yake kwa mfano katika Sha´baan ilikuwa siku saba, basi tutamwambia asubiri siku zengine nane. Baada ya hapo anaweza kuanza kufunga. Ikiwa damu haifanani na damu ya hedhi inapokuja katika rangi yake, harufu yake wala sifa zake, basi hii ni damu ya kawaida ambayo hatakiwi kuizingatia. Kuhusu funga yake katika yale masiku ambayo alikuwa amesafika, funga yake ni sahihi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 19
  • Imechapishwa: 20/03/2022