Swali: Ramadhaan ya mwaka jana sikufunga isipokuwa siku moja peke yake kutokana na maradhi yaliyonipata. Nikifunga katika hali hiyo basi nakuwa mwenye kupooza kabisa na siwezi hata kusimama katika swalah. Ni kipi unachoninasihi hivi sasa kwa kuzingatia kwamba ndio Ramadhaan ya kwanza kupatwa na maradhi haya?

Jibu: Kuna uwezekano maradhi haya yakawa ni maradhi sugu ambayo madaktari wabobezi wana dhana yenye nguvu kwamba hayaponi. Katika hali hiyo inafaa kutofunga. Badala yake utalazimika kulisha chakula kumpa masikini takriban 1½ kg kwa kila siku moja ambayo hukufunga. Chakula kitasimama mahali pa funga, kwa sababu maradhi yake ni sugu yasiyotarajiwa kupona. Kuna uwezekano vilevile maradhi yako ni yenye kupona kwa tawfiyq ya Allaah. Katika hali hiyo utalipa siku hizi 29 pale utakapopona. Vilevile hutolazimika kulisha chakula kwa sababu Allaah (Ta´ala) anasema:

فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi mpya na afunge na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi atimize idadi katika masiku mengine.”[1]

[1] 02:185

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 21
  • Imechapishwa: 20/03/2022