2 – Kuosha mikono hadi kwenye vifundo. Ni kuanzia ncha za vidole hadi mwisho wa vifundo. Vifundo vinaingia kwenye maosho. Kuosha mikono kabla ya kuanza wudhuu´ hakutoshi kama fardhi ya wudhuu´, bali hilo ni jambo linalopendeza, isipokuwa wakati wa kuamka kutoka usingizini, ambapo huwa ni wajibu. Kuosha mikono hufanyika baada ya kuosha uso. Hivyo kilichofanyika kabla ya hapo hakihesabiwi kama sehemu ya fardhi ya wudhuu´.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 15