Faradhi za wudhuu´ ni sita:

1 – Kuosha uso. Mpaka wake kwa urefu ni kutoka mwanzo wa nywele hadi kwenye ndevu zinazoning’inia chini. Upana ni baina ya masikio mawili. Masikio ni sehemu ya kichwa. Kwa msemo mwingine ni kwamba yanafutwa. Si sehemu ya uso na hivyo hayaoshwi.

Kuingiza maji kwenye ndani ya ndevu ni jambo linalopendelewa. Lililo wajibu ni kuosha sehemu ya uso inayotazamana na mtu. Kwa maana nyingine kuchambua ndevu hakuingii katika jambo hilo. Kunaingia katika kuosha uso kusukutua mdomo na kupalizia. Hayo yamebainishwa katika Hadiyth ya ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) na wengineo.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 04/05/2026