14. Du´aa ya kuyaegemeza mambo na kudhihirisha kumuhitaji kwako Allaah

53 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema:

اللَّهُم لَكَ أسْلَمْتُ وبِكَ آمنْتُ، وعليكَ توَكَّلْتُ، وإلَيكَ أنَبْتُ، وبِكَ خاصَمْتُ. اللَّهمَّ أعُوذُ بِعِزَّتِكَ، لا إلَه إلاَّ أنْتَ أنْ تُضِلَّنِي أنْت الْحيُّ الَّذي لاَ تمُوتُ، وَالْجِنُّ وَالإِنْسُ يمُوتُونَ

“Ee Allaah! Kwako nimejisalimisha, Kwako nimeamini, Kwako nimetegemea, Kwako nimetubu na nimegombana kwa ajili Yako. Ee Allaah! Hakika mimi najilinda kwa utukufu Wako, kwani hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe, nisipotee. Hakika Wewe uko Hai ambaye hufi, majini na watu watakufa.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim ambaye tamko ni lake.

MAELEZO

Katika Hadiyth hii kuna kuyaegemeza mambo yako kwa Allaah (´Azza wa Jall). Kwa ajili hiyo ndio maana akasema:

اللَّهُم لَكَ أسْلَمْتُ

“Ee Allaah! Kwako nimejisalimisha… “

Bi maana nimenyenyekea Shari´ah na dini Yako.

وبِكَ آمنْتُ

“Kwako nimeamini.”

Bi maana nimesadikisha.

وإلَيكَ أنَبْتُ

“Kwako nimetegemea.”

Bi maana nimerejea na nimetubu Kwako.

وبِكَ خاصَمْتُ

“Nimegombana kwa ajili Yako.”

Bi maana magomvi yangu ni kwa ajili Yako. Haihusiani na magomvi ya batili, bali ni magomvi ya haki.

اللَّهمَّ أعُوذُ بِعِزَّتِكَ، لا إلَه إلاَّ أنْتَ أنْ تُضِلَّنِي

“Ee Allaah! Hakika mimi najilinda kwa utukufu Wako, kwani hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe, nisipotee.”

Hapa kuna dalili ya mtu kuomba kinga kwa utukufu wa Allaah na kuomba kupitia majina na sifa Zake katika sifa ya uhai. Kuna dalili nyingine ya kumuomba Allaah uongofu na uimara juu ya haki.

[1] al-Bukhaariy (7383) na Muslim (2717).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 60
  • Imechapishwa: 15/10/2025