Swali: Ni ipi bora zaidi kutoa adhaana au kuwa imamu?

Jibu: Kuna maoni kinzani kati ya wanazuoni. Baadhi yao wamependelea upande huu na wengine upande ule. Vyote vina ubora. Lakini udhahiri wa maandiko ni kwamba muadhini ana fadhilah maalum, kwa sababu yeye ndiye anayewaita watu, anawaita kwenda kwa Allaah, anawaita katika kumwabudu Allaah pekee, kumtii Yeye na kusimamisha swalah. Hii ni fadhilah maalum ambayo haikupatikana mfano wake katika uimamu.

Lakini na imamu naye ana fadhilah maalum, kwa sababu imamu ndiye anayewafundisha watu swalah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), anawapa mawaidha na kuwakumbusha. Kwa hiyo imamu akiwa na elimu na ufahamu sahihi, basi ana kheri kubwa ambapo anawakumbusha watu na kujitahidi kuwafikishia haki.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31229/هل-الافضل-الاذان-ام-الامامة
  • Imechapishwa: 19/10/2025