14. ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya Qur-aan

Imaam Ibn Abiy Daawuud (Rahimahu Allaah) amesema:

وقل غيرُ مخلوقٍ كلام مليكنا

03 – Sema “Hayakuumbwa maneno ya Mfalme Wetu”

بذلك دان الأتقياء وأفصحوا

       hivyo ndivyo walivyoamini wachaji Allaah na wakalidhihirisha

MAELEZO

Miongoni mwa ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wakiwemo Maswahabah, wanafunzi zao na wale waliowafuata ni kwamba hawatilii shaka yoyote juu ya kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah ya kihakika. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amezungumza kwayo na akamletea nayo Jibriyl (´alayhis-Salaam). Jibriyl ameyasikia kutoka kwa Allaah na yeye akamteremshia nayo Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo na yeye pia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawafikishia nayo Ummah Wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 64
  • Imechapishwa: 30/12/2023