14. Allaah hasamehi shirki na anasemehe madhambi mengine yote

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚوَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا

 “Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae; na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa hakika amepotoka upotofu wa mbali kabisa.” (04:116)

MAELEZO

Malengo ya mlango huu ni kwamba Bid´ah ni moja katika madhambi makubwa. Kwa sababu Bid´ah zinaipunguza Uislamu, kuzua ndani ya Uislamu na kuutuhumu Uislamu mapungufu kutokana na uzushi na nyongeza hii. Lakini maasi ni kufuata matamanivu na kumtii shaytwaan. Maasi ni mepesi kidogo kuliko Bid´ah na pia mwenye maasi pengine akakimbilia kutubia. Upande wa pili mzushi yeye anaona kuwa ni mzushi na anajiona kuwa ni mwenye kupatia na hatotubia. Mzushi anajiona kuwa ni mwenye kujitahidi na hivyo matokeo yake anaendelea katika Bid´ah. Mzushi yeye anaona kuwa dini yenye mapungufu na ndio maana anaona kuwa anahitajia kuzusha. Kwa ajili hii ndio maana jambo la Bid´ah likawa baya na khatari zaidi kuliko maasi. Allaah amesema kuhusu watenda madhambi:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚوَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا

 “Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae; na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa hakika amepotoka upotofu wa mbali kabisa.”

Watenda maasi wako chini ya matakwa ya Allaah. Kuhusu Ahl-ul-Bid´ah shari yao na khatari yao ni kubwa zaidi. Kwa sababu Bid´ah zao maana yake ni kuutia dosari Uislamu na ndio maana wakaona kuwa wanahitajia uzushi huu. Mtu wa Bid´ah anaona kuwa yuko katika haki na hivyo akaendelea juu yake, akabaki juu yake na yuko tayari kuhoji kwa sababu yake.

Bid´ah haingii ndani ya matakwa ya Allaah. Mwenye nayo ni mwenye kutishiwa Moto isipokuwa ikiwa kama atatubia. Lakini Bid´ah hiyo ikiwa ni chini ya shirki bado kuna matarajio kwa yule mwenye nayo. Kwa sababu Bid´ah hiyo kwa upande fulani itakuwa ni yenye kuingia katika maana ya maasi lakini hata hivyo si yenye kuingia katika maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

 “Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.”

Ikiwa uzushi wa mzushi ni chini ya shirki basi una hukumu moja sawa na maasi kwa upande wa kwamba Allaah hatomdumisha mwenye nayo Motoni.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 02/11/2020