13. Matahadharisho ya kuzua ndani ya dini na mfarakano

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

at-Tirmidhiy ameipokea tena kupitia kwa Abu Hurayrah na akaisahihisha. Lakini hata hivyo ndani yake hakukutajwa Moto, kama ilivyo katika Hadiyth ya Mu´aawiyah inayopatikana kwa Ahmad na Abu Daawuud. Humo mna:

“Katika Ummah wangu watajitokeza watu wanaopatwa na matamanio kama ambavo maradhi ya kichaa yanavompata mwenye nayo; hayatoacha mshila wala kiungo chochote isipokuwa utaingia ndani yake.”[1]

Tafsiri ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) “mwenye kutaka katika Uislamu mwenendo  wa kipindi cha kikafiri” imekwishatangulia.

MAELEZO

Ni lazima kwa waislamu watahadhari na wasizue ndani ya dini na wasifuate mienendo ya kipindi cha kikafiri. Bali ni lazima kushikamana na Uislamu ambao amekuja nao mteule (´alayhis-Salaam), wasaidiane na wausiane. Wafuate yale Allaah ameyaweka katika Shari´ah, wajiepushe na yale Allaah aliyoharamisha na pia wajiepushe na Bid´ah na maasi. Haya ndio yanawawajibikia waislamu, wawe na msimamo na wasaidiane katika wema na kumcha Allaah. Amesema (Ta´ala):

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ

“Saidianeni katika wema na kumcha Allaah.”[2]

وَالْعَصْرِ إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ

“Naapa kwa al-‘Aswr. Hakika ya mwanaadamu bila ya shaka yumo katika khasara. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema na wakausiana kwa kufuata ya haki na wakausiana kuwa na subira.” (103:01-03)

Mfarakano ambapo kila mmoja akashika njia yake ni jambo halijuzu. Mfarakano ni dini ya watu wa kipindi cha kikafiri.

[1] Ahmad (4/102), Abu Daawuud (4597), al-Haakim (1/218) na at-Twabaraaniy (19/376). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwilaal-ul-Jannah” (2).

[2] 05:02

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 02/11/2020