135. Kutoka kwa Allaah kwenda kwa Jibriyl, kutoka kwa Jibriyl kwenda kwa Muhammad

34 – Imaam Abu Bakr bin ´Ayyaash (a.f.k 194).

176 – Haafidhw Abu Haatim ar-Raaziy amesema: Nimemsikia ´Aliy bin Swaalih al-Anmaatwiy: Nimemsikia Abu Bakr bin ´Ayyaash akisema:

”Qur-aan ni maneno ya Allaah ambayo amemkabidhi Jibriyl, ambapo Jibriyl akamkabidhi nayo Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwake ndio imeanza na Kwake ndio itarudia.”[1]

177 – Imaam Abu Daawuud amesema: Hamzah bin Sa´iyd al-Marwaziy ametuhadithia: Nilimuuliza Abu Bakr bin ´Ayyaash, ambaye amesema:

”Yeyote mwenye kudai kuwa Qur-aan ni kiumbe kwa mtazamo wenu ni kafiri zandiki.”[2]

178 – Yahyaa al-Hammaaniy amesema: Abu Bakr bin ´Ayyaash amenihadithia:

”Usiku mmoja nilimwendea Zamzam na nikapewa ndoo ya maziwa na asali.”

179 – Abu Haashim ar-Rifaa´iy amesema: Nimemsikia Abu Bakr akisema:

“Viumbe vimegawanyika katika makundi manne: wenye kupewa udhuru, waliowepesishiwa,  waliotenzwa nguvu na waliopotezwa. Wenye kupewa udhuru ni wanyama, waliowepesishiwa ni wanadamu, waliotenzwa nguvu ni Malaika na waliopotezwa ni Ibliys.”

[1] Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh.

[2] Masaa’il-ul-Imaam Ahmad, uk. 267. Cheni yake ya wapokezi ni nzuri.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 156-157
  • Imechapishwa: 06/01/2025
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy