134. ´Aqiydah ya Sufyaan bin ´Uyaynah

33 – Sufyaan bin ´Uyaynah (107-198), mmoja katika wanazuoni wakubwa.

172 – Ibn Abiy Haatim amesema: Muhammad bin al-Fadhwl bin Muusa ametuhadithia: Muhammad bin Mansuur al-Makkiy al-Jawwaaz ametuhadithia:

”Nilimuona bwana mmoja akimuuliza Sufyaan bin ´Uyaynah: ”Ee Abu Muhammad, unasemaje kuhusu Qur-aan?” Akajibu: ”Ni maneno ya Allaah; yametoka Kwake na Kwake yatarudia.”[1]

173 – Abu Bakr al-Khallaal ametuhadithia: Harb al-Kirmaaniy ametuzindua: Ishaaq bin Raahuuyah ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, ambaye amesema:

”Niliwakuta watu kwa zaidi ya miaka sabini, kuanzia Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wengineo, wakisema: ”Allaah ndiye Muumba na kila kitu kingine ni kiumbe, isipokuwa Qur-aan ambayo ni maneno ya Allaah, Kwake ndio imetoka na Kwake ndio itarudia.'”[2]

Haya yamepokelewa kwa mapokezi mengi kutoka kwa Ibn ´Uyaynah.

174 – Abu Bakr as-Swaghaaniy amesema: Luwayn ametuhadithia:

”Ibn ´Uyaynah aliulizwa: ”Nini kinachosemwa kuhusu Hadiyth hizi ulizopokea juu ya Kuonekana?” Akajibu: ”Ni za kweli. Tumezisikia kutoka kwa watu ambao tunawaamini na kuwaridhia.”

175 – Ahmad bin ad-Dawraqiy amesema: Ahmad bin Naswr amenihadithia:

”Baada ya kumuuliza Sufyaan bin ´Uyaynah kwa king´ang´anizi nikamsikia anasema nyumbani kwake baada ya ´Ishaa:

”Niache nipumue.” Nikasema: ”Ee Abu Muhammad! Kuna jambo nataka kukuuliza.” Akasema: ”Usiulize.” Nikasema: ”Lazima nikuulize. Vinginevyo nimuulize nani?” Akasema: ”Hebu.” Nikasema: ”Ni vipi kuhusu Hadiyth kutoka kwa ´Ubaadah, kutoka kwa ´Abdullaah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Je, umepata khabari kwamba Allaah (´Azza wa Jall) ataziweka mbingu kwenye kidole, ardhi kwenye kidole… ”

”Hakika nyoyo za wanadamu ziko kati ya vidole viwili katika vidole vya Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall)… ”

”Allaah (´Azza wa Jall) anastaajabu na kucheka.”?

Sufyaan akasema: ”Ni kama zilivyopokelewa. Tunazithibitibisha na kuzisimulia bila kuzifanyia namna.”

[1] Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh.

[2] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Wasimulizi wake walikuwa wenye kuhifadhi na watu madhubuti. al-Bukhaariy amesema: al-Hakam bin Muhammad at-Twabariy amenihadithia, kitu nilichokiandika kutoka kwake Makkah: ”Sufyaan bin ´Uyaynah ametuhadithia:

”Niliwakuta wanazuoni wetu kwa zaidi ya miaka sabini, akiwemo ´Amr bin Diynaar, wakisema kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah na si kiumbe.” (Khalqu Af´aal-il-´Ibaad (1))

Cheni yake ya wapokezi ni nzuri.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 155-156
  • Imechapishwa: 06/01/2025
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy