35 – ´Aliy bin ´Aaswim, msomi wa Hadiyth wa Waasitw (108-201).

180 – Yahyaa bin ´Aliy bin ´Aaswim amesimulia:

“Usiku mmoja nilikuwa kwa baba yangu ambapo al-Maariysiy akaomba idhini ya kuingia kwake. Nikamwambia: ”Ee baba yangu kipenzi, unamwacha mtu kama huyu kuja kwako?” Akasema: ”Ana nini?” Nikamwambia: ”Anasema kuwa Qur-aani ni kiumbe na anadai kwamba Allaah yuko pamoja   naye ardhini.” Sikuwahi kumuona baba yangu akikasirika sana kama alivyosikia kwamba mtu huyo anasema eti Allaah yuko pamoja naye ardhini na kwamba eti Qur-aan imeumbwa.”[1]

181 – ´Aliy bin ´Aaswim amesema:

“Wakati niliposafiri baba yangu alinipa dinari 100 000. Wakati niliporudi kutoka safari yangu, nilikuwa nimeandika Hadiyth 100 000.”

Alikuwa bahari ya elimu. Aliishi miaka 94. Hata hivyo alikabiliwa na udhaifu katika usimulizi wa Hadiyth.

[1] Simjui ni nani huyu Yahyaa bin ´Aliy bin ´Aasim. Hakutajwa katika wasimulizi wa ´Aliy bin ´Aaswim.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 157
  • Imechapishwa: 06/01/2025
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy