36 – Shaykh-ul-Islaam Yaziyd bin Haaruun (a.f.k 206).
182 – Shaadh bin Yahyaa amehadithia kwamba amemsikia Yaziyd bin Haaruun akiulizwa swali lifuatalo:
”Jahmiyyah ni watu gani?” Akajibu: “Wale wenye kusema kuwa mwingi wa Rehema amelingana juu ya ´Arshi kwa namna isiyofahamika na kile kilicho imara katika mioyo ya watu wa kawaida, huyo ni Jahmiy.”[1]
Wakusudiwao ni kikosi kikubwa cha ummah na wanazuoni. Kile kilicho imara ndani ya nyoyo zao katika Aayah ni yaliyofahamishwa na uzungumzishwaji. Aidha yakini yao kwamba Yule ambaye amelingana juu ya ´Arshi hakuna chochote mfano Wake. Hiki ndicho kilichokita mizizi katika maumbile yao safi na akili zao sahihi. Haya ndio yaliyojidhatiti ndani ya maumbile yao yaliyosalimika na akili zao timamu. Kama kungekuwa na maana nyingine zaidi ya hiyo, basi wangeiandika waziwazi na wasingeipuuza. Na kama mmoja wao angefasiri Kulingana juu, basi juhudi zingefanyika kuhakikisha maana hiyo inasambazwa, na kama ingeenezwa, basi ingetambulika. Ikiwa kuna baadhi ya wajinga miongoni mwa wapumbavu wanaoelewa Kulingana juu kwa namna inayopelekea upungufu au kufananisha baina ya kilichopo mbele na kisichoonekana au kiumbe na Muumba, basi hali hii ni nadra. Na yeyote anayesema hivyo anapaswa kuonywa na kufundishwa. Sidhani kama kuna yeyote katika watu wa kawaida ambaye anafahamu kwa njia hiyo – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
[1]Ameipokea ´Abdullaah bin Ahmad katika “as-Sunnah”, uk. 11-12, na kupitia kwake ameisimulia mtunzi wa kitabu. Hapa, na maeneo mengine, ametaja kitabu chake “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” na akasema: ´Abdullaah amesema: ´Abbaas bin ´Abdil-´Adhwiym al-´Anbariy amenihadithia: Shaadh bin Yahyaa ametuhadithia…
Abu Daawuud ameipokea katika “Masaa’il-ul-Imaam Ahmad”, uk. 268, na akasema: Ahmad bin Sinaan ametuhadithia: Nimemsikia Shaadh bin Yahyaa…
Cheni hii ya wapokezi ni nzuri. Kuna watu wengi madhubuti wamenukuu kutoka kwa Shaadh bin Yahyaa na Ahmad pia alimzungumzia kwa wema. al-Bukhaariy ameyanukuu masimulizi haya kwa cheni ya wapokezi pungufu na akasema:
”Yaziyd bin Haaruun alitawahadharisha Jahmiyyah na akasema: “Wale wenye kusema kuwa mwingi wa Rehema amelingana juu ya ´Arshi kwa namna isiyofahamika na kile kilicho imara katika mioyo ya watu wa kawaida, huyo ni Jahmiy.” (Khalqu Af´aal-il-´Ibaad (63))
- Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 157-158
- Imechapishwa: 06/01/2025
- taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy

Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 157-158
Imechapishwa: 06/01/2025
taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
https://firqatunnajia.com/137-aqiydah-ya-mtu-mwenye-maumbile-na-akili-timamu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)