134. Moyo tu ambayo umetiwa nuru ndio unaona jambo hili

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Hadiyth inaamrisha kujitofautisha nao. Hiyo maana yake ni kuwa kujitofautisha nao ni lengo la Shari´ah. Ikiwa amri ya kujitofautisha nao ni lengo, ijapo ni kubadilisha mvi peke yake, ni kwa sababu ya kule kujitofautisha katika amri. Kujitofautisha ima ikawa ni sababu yenyewe, sababu nyingine au sehemu ya sababu. Kwa makadirio yote, kujitofautisha ni lengo limeamrishwa na linalotakakikana katika Shairi´ah.”[1]

Kisha akataja faida za kipekee na za kielimu kisha akasema:

”Hata kama inafahamisha kuwa kujitofautisha nao ni lengo linatakikana katika Shari´ah, hiyo haina maana kuwa amri yenyewe haina manufaa mengine. Hapa tuna mambo mawili:

1 – Kujitofautisha na namna ya kuishi kwao kidhahiri kuwanufaisha waja wa Allaah waumini ambapo kuna kujitenga mbali na matendo yanayofanywa na wakazi wa Motoni. Hata hivyo, manufaa hayo yanaonekana na yule ambaye moyo wake umetiwa nuru mpaka akaona jinsi wale watu walioghadhibikiwa na waliopotea wanavyosumbuliwa na maradhi ambayo madhara yake ni makubwa zaidi kuliko madhara ya magonjwa ya miili.

2 – Mtindo wao wa maisha na muonekano wao kunaweza kuwa ima na madhara au na mapungufu, kwa ajili ndio maana kumekatazwa. Badala yake kukaamrishwa kinyume chake kutokana na yale manufaa na ukamilifu uliyomo ndani yake. Mtindo wa maisha yao ima ukawa na madhara peke yake au mapungufu. Kwa sababu yale walionayo si vyengine isipokuwa tu ni mambo yaliyozuliwa, yaliyofutwa na mfano wake ambayo ni madhara matupu. Na yale walionayo ambayo hayakufutwa yameongezwa au kupunguzwa. Kwa hivyo kujitafautisha nao ni kwa maana ya kwamba jambo limewekwa katika Shari´ah kikamilifu – na kwamba kuna jambo ambalo linatokana nao ambalo limekamilika ni kitu kisichoingia akilini. Kwa sababu sisi tunanufaika na kule kujitofautisha nao katika mambo yote. Hata yale mambo yao ya kidunia ambayo wako mairi yanaweza kuwa yenye kuwadhuru huko Aakhirah au pia yanadhuru yale mambo ya kidunia ambayo ni muhimu zaidi. Kwa hiyo kujitofautisha nao kuna manufaa kwetu.

Baada ya yote, matendo na mambo yote kimaisha ya kafiri ni lazima yawe na kasoro inayowazuia kutonufaika nayo. Na kama kuna jambo la kimanufaa la kidunia ambalo limekamilika, basi hastahiki kwa jambo hilo malipo huko Aakhirah. Lakini mambo yake yote ima yakawa yameharibika au yakawa na mapungufu. Himdi zote njema anastahiki Allaah juu ya neema ya Uislamu ambayo ndio neema kubwa kabisa. Uislamu ndio msingi wa kheri zote anazozipenda Mola wetu na kuziridhia. Hakika imekwishabainika kuwa kujitofautisha nao ni lengo linalotakikana katika Shari´ah kwa jumla. Kwa ajili hiyo Imaam Ahmad na wengineo walikuwa wakitoa sababu ya kujifautisha kwa kule kuzipaka rangi nywele.”[2]

Halafu akataja baadhi ya nukuu juu ya hilo kutoka kwa Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah).

[1] Iqtidhwaa’-us-Swiraat al-Mustaqiym, uk. 24

[2] Iqtidhwaa’-us-Swiraat al-Mustaqiym, uk. 27

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 188-189
  • Imechapishwa: 19/11/2023