Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
108 – Kujiaminisha na kukata tamaa yote yanamtoa mtu nje ya Uislamu.
MAELEZO
Miongoni mwa misingi mikubwa ya ´Aqiydah ya kiislamu ni kuwa na khofu na kutaraji. Ni lazima kukusanya yote mawili. Haitoshi kutosheka na kimoja wapo. Allaah (Ta´ala) amesema alipokuwa akiwasifu Mitume Wake:
إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ
“Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri na wakituomba kwa matumaini na khofu na walikuwa Kwetu wenye kunyenyekea.”[1]
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ ۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحْذُورًا
“Hao wanaowaomba [wao wenyewe] wanatafuta kwa Mola wao njia [na] kumkurubia kadri wanavyoweza na wanataraji rehema Zake na wanakhofu adhabu Yake. Hakika adhabu ya Mola wako ni ya kutahadhariwa daima.”[2]
Walikuwa wakikusanya kukhofu na kutaraji. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
أَمَّنْ هُوَ قَانِتٌ آنَاءَ اللَّيْلِ سَاجِدًا وَقَائِمًا يَحْذَرُ الْآخِرَةَ وَيَرْجُو رَحْمَةَ رَبِّهِ
“Je, yule anayeshikamana na ‘ibaadah nyakati za usiku hali ya kusujudu na kusimama ilhali anatahadhari na Aakhirah na anataraji rehema ya Mola wake?”[3]
Vilevile ni lazima mtu ampende Allaah. Ni lazima yapatikane mambo haya matatu:
1 – Kumpenda Allaah.
2 – Kumuogopa Allaah.
3 – Kutaraji thawabu Zake.
Yule anayependa peke yake ni Suufiy. Suufiyyah wanamwabudu Allaah (´Azza wa Jall) kwa mapenzi; hawamuogopi na wala hawatarajii thawabu Zake. Wanasema kuwa hawamwabudu Allaah kwa sababu ya kutaka kuingia Peponi au kutaka kuepukana na Moto – wanasema kuwa wanamwabudu kwa sababu tu wanampenda. Fikira hiyo ni upotevu.
Yule anayemwabudu Allaah kwa khofu peke yake ni Khaarijiy. Khawaarij wamechukuaupande wa khofu na makemeo peke yake. Ndio maana wakakufurisha kwa madhambi.
Yule anayemwabudu Allaah kwa matarajio peke yake ni Murjiy´. Murji-ah wamechukua upande wa matarajio peke yake na wakaacha upande wa khofu.
Kuhusu wapwekeshaji, wanamwabudu Allaah kwa mambo yote matatu: kwa mapenzi, khofu na matarajio.
[1]21:90
[2]17:57
[3]39:9
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 141-143
- Imechapishwa: 18/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)