Maana ya maafikiano upande wa lugha ni maazimio na makubaliano. Maana ya istilahi ni maafikiano ya wanazuoni Mujtahiduun katika Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya hukumu ya ki-Shari´ah baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maafikiano ni hoja. Amesema (Ta´ala):

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللّهِ وَالرَّسُولِ

“Na mkizozana katika jambo lolote, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ummah wangu hauafikiani juu ya upotofu.”[2]

Ameipokea at-Tirmidhiy.

[1] 04:59

[2] at-Tirmidhiy (2167), Ibn Abiy ´Aaswim katika ”as-Sunnah” (80), al-Haakim (01/115, 116), al-Khatwiyb katika ”al-Faqiyh wal-Mutafaqqah” (01/61). at-Tirmidhiy amesema: ”Hadiyth ni geni.” Cheni ya wapokezi wake ni dhaifu, kama ilivyo katika Takhriyj-us-Sunnah (01/40) ya al-Albaaniy. Hadiyth inayo njia nyingine kwa at-Twabaraaniy katika ”al-Kabiyr” (12/447) kwa cheni ya wapokezi nzuri. al-Haythamiy amesema katika ”al-Majma´ (05/218): ”Ameipokea at-Twabaraaniy kwa sanadi mbili. Wanamme wa moja wapo ni wanamme wa “as-Swahiyh” isipokuwa tu Marzuuq ambaye ni mtumwa huru wa kizazi cha Twalhah. Lakini ni mwaminifu.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 165
  • Imechapishwa: 22/02/2023