Maneno yake mtunzi:

“Wanaotofautiana ni wenye kusifiwa kwa kutofautiana kwao.”

Haina maana kuwa kunasifiwa kule kutofautiana. Kukubaliana ni bora kuliko kutofautiana. Hakika si venginenvyo makusudio ni makatazo ya kuwasema vibaya na kwamba kila mmoja ni mwenye kusifiwa kwa aliyoyasema. Kwani mwenye kujitahidi amekusudia haki. Kwa hivyo ni mwenye kusifiwa kwa kujitahidi kwake na kufuata ile haki iliyomdhihirikia ijapo hakupatia haki yenyewe.

Maneno yake mtunzi:

“Tofauti katika matawi ni rehema na tofauti yao ni rehema kunjufu.”

Inaingia ndani ya rehema na msamaha wa Allaah kwa vile hakuwakalifisha zaidi ya vile walivyoweza na hakuwalazimisha zaidi ya kile kilichowadhihirikia. Kwa hivyo hawana neno juu ya tofauti hii. Bali wanaingia ndani ya rehema na msamaha wa Allaah. Wakipatia basi wanapata thawabu mara mbili na wakikosea wanapata thawabu mara moja.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 164-165
  • Imechapishwa: 22/02/2023