Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Hakuna katika akili timamu wala nukuu za kiwahy chochote kinachopingana na ´Aqiydah ya Salaf. Hata hivyo wakati na mahali si pake kuraddi hoja tata hiyo. Yule ambaye moyoni mwake mna hoja tata na akataka kuitatua, basi hilo ni sahali na rahisi.

MAELEZO

Nukuu sahihi ni ile isiyokuwa na mashaka na dhana potofu. Nukuu sahihi ni iliyokuja na Qur-aan au Sunnah Swahiyh. Hakuna ndani yake chochote kinachopingana na njia ya Salaf kabisa.  Bali njia ya Salaf inaenda sambamba na akili timamu na nukuu sahihi. Ama hawa wapotofu, wao wanapingana na nukuu sahihi na akili timamu. Ikiwa zitapingana, basi huenda akili siyo timamu au nukuu siyo sahihi.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 220
  • Imechapishwa: 12/07/2026