Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Haki ni ile waliyoafikiana kwayo wabora wa ummah; kwamba Allaah amelingana juu ya ´Arshi kulingana ambako kunaendana na utukufu Wake. Kama ambavo anasifiwa kuwa juu ya kila jambo ni Mjuzi, juu ya kila jambo ni Muweza, kwamba ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona kwa njia isiyolingana na sifa za viumbe, basi vivyo hivyo Yeye (Subhaanah) yuko juu ya ´Arshi kwa njia isiyolingana na ujuu wa viumbe – Allaah ametakasika kutokamana na jambo hilo!
MAELEZO
Kwa maana kwamba yale waliyoafikiana kwayo Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. ´Aqiydah yao ni kusimama kwenye yale yaliyokuja katika Qur-aan na Sunnah bila kuingiza ndani yake mawazo na akili. Bali tunathibitisha yale ambayo Allaah amejithibitishia Mwenyewe au aliyomthibitishia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa mujibu wa vile ilivyokuja katika dalili. Tunathibitisha maana yake kwa mujibu wa lugha ambayo Qur-aan imeteremshwa kwayo. Wala hatuvuki zaidi ya hapo, kwa sababu hayo ni katika elimu ya ghaibu ambayo hakuna aijuaye isipokuwa Allaah:
يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا
“Anajua yale yaliyoko mbele yao na yale yaliyoko nyuma yao na hawawezi kumzunguka kwa kumtambua.”[1]
Usiifanye ujuzi wa Muumba kama ujuzi wa kiumbe, wala uwezo wa Muumba kama uwezo wa kiumbe. Bali uwezo na ujuzi wa Muumba ni maalum Kwake. Vivyo hivyo kiumbe dhaifu kina uwezo, ujuzi na sifa zinazokihusu.
Amelingana (Subhaanahu wa Ta´ala) juu ya ´Arshi. Kulingana Kwake juu ya ´Arshi kunapelekea kwamba Yuko juu ya ´Arshi:
إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ
“Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi.”[2]
Kwa maana kwamba Yuko juu ya ´Arshi. Je, kuwa Kwake juu ya ´Arshi ni kama kuwa kwa kiumbe juu ya kitanda au juu ya paa? Sivyo kabisa. Kwa sababu kiumbe huhitaji kilicho chini yake kimbebe. Hivyo Allaah (´Azza wa Jall) halinganishwi kabisa na viumbe Wake. Kwa hiyo kulingana Kwake juu, ujuzi, uwezo Wake, dhati Yake, majina Yake na sifa Zake ni maalum Kwake na zinalingana na Yeye tu (Subhaanahu wa Ta´ala). Hazifanani kabisa na sifa na majina ya viumbe, wala sifa zao maalum na yale yanayopelekea.
[1] 20:110
[2] 07:54
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 219-220
- Imechapishwa: 12/07/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 219-220
Imechapishwa: 12/07/2026
https://firqatunnajia.com/131-hatuvuki-zaidi-ya-hapo/