130. Kama mwanadamu anavyokaa juu ya kiti?

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Aidha anasema kuwa ikiwa Allaah amelingana juu ya ´Arshi, basi anafanana na namna ambavyo mtu anakaa juu ya kiti na ndani ya safina – kwa sababu ndio kulingana pekee kunakofahamika. Anayefikiria namna hiyo hakuna kingine anachofahamu isipokuwa isipokuwa kulingana kwa kiumbe.

MAELEZO

Hizi ni katika tafsiri zao za batili. Wanasema ikiwa tukithibitisha kulingana juu kwa Allaah, basi itawalazimu kwamba Allaah anaihitajia ´Arshi, kama vile mwanadamu anavyohitaji kitanda ili alale juu yake, akae juu yake, kiti, paa, jahazi au mnyama. Kiumbe huhitaji vitu hivi. Lakini Muumba hahitaji vitu hivi. Bali vitu hivi ndivyo vinavyomhitaji Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ama Allaah, Yeye ni Mkwasi kuvihusu na kuvihusu vinginevyo. Basi vipi mnampima mwenye kuhitaji kwa dhati yake na Yule Mkwasi kwa dhati Yake? Hii ni kosa.

Kwa msingi huo wakakanusha kulingana juu kwa Allaah, kwa sababu hawakuelewa isipokuwa kulingana juu kwa kiumbe juu ya kiumbe kingine. Hivyo wakaikanusha kwa madai eti ya kumtakasa Allaah. Ufahamu wenu huu ni kosa kuanzia asili yake, kwa sababu jambo hilo halilazimiki. Wala hamkujua haki ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) wala hamkumtukuza Allaah inavyostahiki. Bali nyinyi mmemfanya kama kiumbe – Allaah ametukuka kutokana na hilo!

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 217
  • Imechapishwa: 12/07/2026