Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Anayesema hivi anafanana na yule mwenye kusema kwamba ikiwa walimwengu wana Muumba, basi ima awe dutu au isiyo ya kimwili[1] – yote mawili ni mambo yasiyowezekana Kwake. Kwa sababu hakuna kilichopo isipokuwa ima kiwe moja ya hayo mambo mawili.
MAELEZO
Dutu ni kile kinachosimama chenyewe, isiyo ya kimwili ni kile kisichosimama chenyewe, mfano wa rangi na harufu. Allaah (´Azza wa Jall) ametakasika na haya, kwa sababu jambo hili halikuja katika Qur-aan wala Sunnah. Hivyo sisi tunanyamaza kuhusu hilo. Taswira hii ipo kwa viumbe. Kiumbe lazima awe dutu au asiye na mwili. Ama Muumba (´Azza wa Jall), jambo hili halilazimiki katika haki Yake. Wao daima wanamlinganisha Muumba kwa viumbe na ndiyo maana wamepotea. Lau wangefuata ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah na kusema sifa za Muumba hazilazimiki kuwa kama sifa za viumbe basi wangesalimika na haya yote. Amesema (Ta´ala):
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye.”[2]
وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
“Na wala hana yeyote anayefanana [na kulingana] Naye.”[3]
[1] Dutu ni kile kinachokubali kuwa na ukomo na isiyo ya kimwili ni kile kisichosimama kwa dhati yake, bali husimama kwa kitu kingine. Tazama ”Ghaayat-ul-Maraam”, uk. 179, ya al-Aamidiy, ”Maqaalaat-us-Islaamiyyiyn”, uk. 301, na ”al-Jawaab as-Swahiyh” (5/6).
[2] 42:11
[3] 112:4
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 216
- Imechapishwa: 12/07/2026
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Anayesema hivi anafanana na yule mwenye kusema kwamba ikiwa walimwengu wana Muumba, basi ima awe dutu au isiyo ya kimwili[1] – yote mawili ni mambo yasiyowezekana Kwake. Kwa sababu hakuna kilichopo isipokuwa ima kiwe moja ya hayo mambo mawili.
MAELEZO
Dutu ni kile kinachosimama chenyewe, isiyo ya kimwili ni kile kisichosimama chenyewe, mfano wa rangi na harufu. Allaah (´Azza wa Jall) ametakasika na haya, kwa sababu jambo hili halikuja katika Qur-aan wala Sunnah. Hivyo sisi tunanyamaza kuhusu hilo. Taswira hii ipo kwa viumbe. Kiumbe lazima awe dutu au asiye na mwili. Ama Muumba (´Azza wa Jall), jambo hili halilazimiki katika haki Yake. Wao daima wanamlinganisha Muumba kwa viumbe na ndiyo maana wamepotea. Lau wangefuata ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah na kusema sifa za Muumba hazilazimiki kuwa kama sifa za viumbe basi wangesalimika na haya yote. Amesema (Ta´ala):
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye.”[2]
وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
“Na wala hana yeyote anayefanana [na kulingana] Naye.”[3]
[1] Dutu ni kile kinachokubali kuwa na ukomo na isiyo ya kimwili ni kile kisichosimama kwa dhati yake, bali husimama kwa kitu kingine. Tazama ”Ghaayat-ul-Maraam”, uk. 179, ya al-Aamidiy, ”Maqaalaat-us-Islaamiyyiyn”, uk. 301, na ”al-Jawaab as-Swahiyh” (5/6).
[2] 42:11
[3] 112:4
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 216
Imechapishwa: 12/07/2026
https://firqatunnajia.com/129-wao-daima-wanamfananisha-muumba-na-viumbe/