Kumkumbusha mgonjwa juu ya Allaah

Swali: Ikiwa muumini atamtembelea mgonjwa ni du´aa gani amuombee? Ni du´aa gani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliomba alipomtembelea mgonjwa?

Jibu: Alipomtembelea mgonjwa alisema:

لا بأس طهور إن شاء الله

“Hakuna neno [ugonjwa] ni kusafishwa na [madhambi] – Allaah akitaka.”

Kwa hiyo aseme hivo na amwombee rehema, afueni na kupona. Hili ndilo lililowekwa katika Shari´ah. Akimtembelea amuombee afueni na kupona. Aidha atamshauri juu ya kumcha Allaah na subira. Vilevile atamkumbusha kwamba magonjwa ni kafara na hupunguza madhambi. Amkumbushe juu ya Allaah na amtie moyo na amuombee kupona na kwamba ugonjwa wake uwe utakaso na kafara.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1246/الدعاء-الوارد-في-زيارة-المريض
  • Imechapishwa: 11/07/2026