Swali: Ikiwa mwanamke anakubaliana kutopata ujauzito kwa kutumia vidonge vya kuzuia mimba. Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Kutumia vidonge vya kuzuia uzazi kunahitaji ufafanuzi. Ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo, kwa mfano mke anapata mimba kila baada ya muda mfupi na jambo hilo linamdhuru, basi hakuna tatizo kutumia vidonge ilimradi tu viwe salama kwake na matumizi yake yawekwe chini ya uangalizi wa daktari na awe na ujuzi wa namna ya kuvitumia. Anaweza kutumia kwa muda kama mwaka, miaka miwili au zaidi kulingana na haja, kisha aache ili apate ujauzito na yeye pamoja na mumewe wanufaike vilevile waislamu kwa ujumla. Haifai kutumia vidonge hivyo kwa kudumu bila haja maalum, bali vitumike kwa kadiri ya haja tu. Au kama ana maradhi yanayomdhuru akipata mimba, kwa mfano hawezi kujifungua isipokuwa kwa upasuaji unaomdhuru sana, basi anaweza kutumia vidonge kwa sababu ya madhara hayo makubwa au kwa sababu nyingine zinazokubalika katika Shari´ah.
Ama kuzoea kutumia vidonge bila sababu maalum, haifai. Jambo hilo lina madhara kwa jamii na linapingana na hekima aliyoiweka Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kupitia ulimi wa Mtume wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kuhimiza kuongezeka kwa watoto ili kuongeza idadi ya ummah. Makafiri na washirikina hupenda watu watumie vidonge hivyo ili kupunguza kizazi cha waislamu na kuongeza idadi ya maadui zao. Hivyo haifai muislamu kutimiza matakwa ya makafiri kwa kutumia vidonge vinavyodhuru jamii na kupunguza kizazi cha waislamu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1178/استعمال-حبوب-منع-الحمل-لعدم-الانجاب
- Imechapishwa: 11/07/2026
Swali: Ikiwa mwanamke anakubaliana kutopata ujauzito kwa kutumia vidonge vya kuzuia mimba. Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Kutumia vidonge vya kuzuia uzazi kunahitaji ufafanuzi. Ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo, kwa mfano mke anapata mimba kila baada ya muda mfupi na jambo hilo linamdhuru, basi hakuna tatizo kutumia vidonge ilimradi tu viwe salama kwake na matumizi yake yawekwe chini ya uangalizi wa daktari na awe na ujuzi wa namna ya kuvitumia. Anaweza kutumia kwa muda kama mwaka, miaka miwili au zaidi kulingana na haja, kisha aache ili apate ujauzito na yeye pamoja na mumewe wanufaike vilevile waislamu kwa ujumla. Haifai kutumia vidonge hivyo kwa kudumu bila haja maalum, bali vitumike kwa kadiri ya haja tu. Au kama ana maradhi yanayomdhuru akipata mimba, kwa mfano hawezi kujifungua isipokuwa kwa upasuaji unaomdhuru sana, basi anaweza kutumia vidonge kwa sababu ya madhara hayo makubwa au kwa sababu nyingine zinazokubalika katika Shari´ah.
Ama kuzoea kutumia vidonge bila sababu maalum, haifai. Jambo hilo lina madhara kwa jamii na linapingana na hekima aliyoiweka Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kupitia ulimi wa Mtume wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kuhimiza kuongezeka kwa watoto ili kuongeza idadi ya ummah. Makafiri na washirikina hupenda watu watumie vidonge hivyo ili kupunguza kizazi cha waislamu na kuongeza idadi ya maadui zao. Hivyo haifai muislamu kutimiza matakwa ya makafiri kwa kutumia vidonge vinavyodhuru jamii na kupunguza kizazi cha waislamu.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1178/استعمال-حبوب-منع-الحمل-لعدم-الانجاب
Imechapishwa: 11/07/2026
https://firqatunnajia.com/wanandoa-wamekubaliana-kutumia-vidonge-vya-kuzuia-mimba/