13. Unasemaje juu ya anayewaita Salafiyyuun kwamba ni Zalafiyyuun?

Swali 13: Kuna vijana ambao wanawaita wanafunzi wa Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy na wa Shaykh Swaalih as-Suhaymiy ya kwamba ni “Zalafiyyuun” (زَلَفَىين) na kwamba sio Salafiyyuun. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Haya ni matusi yanayoelekezwa kwa Salafiyyuun na khaswa inapokuja kwa watu hawa. Ni dalili yenye kufahamisha ukhabithi wao. Watu hawa wameyaelekeza matusi, chuki na njama zao zote kwa Salafiyyuun wanaomuabudu Allaah peke yake.  Pamoja na haya yote watu hawa wanashirikiana na makundi yote yaliyozuliwa. Bali wanashirikiana mpaka na Raafidhwah. Matendo na maneno yao haya ni batili. Hayajuzu. Uhakika wa mambo ni kuwa uharibifu ni yale wanayoyafanya, Hizbiyyah wanayoiamini na kufuata maoni ya viongozi wao.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 16/07/2017