Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Nguzo za swalah ni kumi na nne:
1- Kusimama kwa mwenye kuweza.
2- Takbiyr ya kufungulia swalah.
3- Kusoma al-Faatihah.
4- Rukuu´.
5- Kuinuka kutoka katika Rukuu´.
6- Kusujudu juu ya viungo saba.
7- Kuinuka kutoka katika Sujuud.
8- Kukaa baina ya Sajdah mbili.
9- Utulivu katika nguzo zote.
10- Kupangilia.
11- Tashahhud ya mwisho.
12- Kukaa katika Tashahhud ya mwisho.
13- Kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
14- Tasliym.
MAELEZO
Hapa mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) anabainisha nguzo za swalah. Ameingiza kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa ni moja katika nguzo za swalah. Nguzo hizo ni:
1- Kusimama kwa mwenye kuweza.
2- Takbiyr ya kufungulia swalah.
3- Kusoma al-Faatihah.
4- Rukuu´.
5- Kuinuka kutoka katika Rukuu´.
6- Kusujudu juu ya viungo saba.
7- Kuinuka kutoka katika Sujuud.
8- Kukaa baina ya Sajdah mbili.
9- Utulivu katika nguzo zote.
10- Kupangilia.
11- Tashahhud ya mwisho.
12- Kukaa katika Tashahhud ya mwisho.
13- Kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
14- Tasliym.
Nguzo ni kitu ambacho ni lazima kipatikane na hakianguki si kwa kukusudia wala kwa kusahau. Tofauti kati ya nguzo na mambo ya wajibu ni kwamba jambo la wajibu linaanguka kwa kusahau au kwa kutokujua. Kuhusu nguzo ni kitu ambacho hakianguki si kwa kusahau, kwa kutokujua wala kwa kukusudia. Hilo linafahamishwa na Hadiyth ya yule mtu aliyeswali vibaya na akafunzwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Pindi aliposwali kimakosa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia:
”Unaposimama kwa ajili ya swalah, basi timiza vizuri wudhuu´ wako. Halafu elekea Qiblah na kusema ”Allaahu Akbar”. Halafu soma kile kitachokuwepesikia katika Qur-aan… ”[1]
Nguzo hizi kumi na nne zitatajwa huko mbeleni kwa maelezo.
[1] al-Bukhaariy (6251).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 96-98
- Imechapishwa: 01/07/2018
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related

Sehemu za kupandisha mikono katika swalah
https://www.youtube.com/watch?v=eWJ2EMkXsTY Swali: Je, ni wajibu kupandisha mikono wakati wa Takbiyrat-ul-Ihraam tu au ni lazima kuipandisha katika nguzo zote za Swalah? Jibu: Sunnah ni kupandisha mikono wakati wa Ihraam, na wakati wa Rukuu´, na wakati wa kutoka katika Rukuu´ na wakati wa kusimama kutoka katika Tashahhud ya kwanza mpaka ya tatu.…
In "Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz"
53. Nguzo ya nne: Rukuu´
Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema: Halafu mtu anaenda kwenye Rukuu´, kuinuka kutoka kwenye Rukuu´, kunyooka sawasawa, kusujudu juu ya viungo saba na kuinuka kutoka hapo na kukaa baina ya Sajdah mbili. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala): يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ارْكَعُوا وَاسْجُدُوا “Enyi mloamini! Rukuuni na…
In "Sharh Shuruwt-is-Swalaah - ar-Raajihiy"
04. Sababu ya pili ambayo ni kupunguza
2 - Kupunguka 1 – Kupunguza nguzo: Mwenye kuswali pale ambapo atapunguza nguzo katika swalah yake, ikiwa ni Takbiyrat-ul-Ihraam, basi swalah si sahihi. Ni mamoja ikiwa ameiacha kwa kusahau au kwa kukusudia. Kwa sababu swalah yake haikufungika. Ikiwa ni kitu kingine kisichokuwa Takbiyrat-ul-Ihraam na akawa amekiacha kwa kukusudia, basi swalah…
In "Sujuud-us-Sahw - Ibn ´Uthaymiyn"