13. Naweza kukata swawm nikisafiri 90 km kwenda kazini?

Swali 13: Inafaa kwangu kukata swawm ikiwa nasafiri kazini 90 km kutoka nyumbani kwangu?

Jibu: Ndio. Umbali huu unazingatiwa kuwa ni safiri. Inafaa kwako kukata swawm hata kama vyombo vya safiri leo ni rahisi na raha. Hii ni ruhusa kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ni swadaqah Allaah aliyokupeni. Hivyo basi ichukueni swadaqah yake.”[1]

[1] Muslim (686).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 28
  • Imechapishwa: 12/06/2017