14. Mwanamke anaweza kuswali na kufunga damu yake ikikatika siku mbili?

Swali 14: Kuna mwanamke alizaa na damu ikaendelea siku arubaini. Kisha damu ikakatika siku mbili. Halafu ikarudi tena. Je, alitakiwa kuswali na kufunga katika siku hizi mbili?

Jibu: Asiswali na wala asifunge isipokuwa baada ya damu yake kukatika kabisa kabisa. Ni jambo linalojulikana kuwa mwishoni wa nifasi damu yake hukatika siku mbili au tatu halafu inarudi. Midhali damu yake inakwenda na kurudi asiswali wala asifunge. Nifasi yake itapokatika kabisa hapo ndipo anatakiwa kujitwaharisha, kuswali na kufunga.

Kujengea juu ya hili swalah yake na swalah yake si sahihi. Kama alifunga basi ni juu yake kulipa tena. Mwanamke mwenye hedhi anayejua hedhi yake hatakiwi  kufanya haraka. Damu huja na kwenda. Asubiri mpaka pale atapoona vizuri umanjano.

Alama ya kutwaharika inajulikana kwa njia mbili:

1- Damu kukatika.

2- Umanjano.

Umanjano ni majimaji yanayomtoka mwanamke na ni alama juu ya kutwaharika kwake. Yakimtoka ni alama ya kutwaharika. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alikuwa akiwaambia wanawake:

“Msiwe na haraka mpaka muone manjano ya wazi.”[1]

Hapo ndipo ataoga, ataswali, atafunga, kugusa Qur-aan na kutembelea msikiti. ´Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Tulikuwa hatuzingatii umanjano na uchafu baada ya kutwaharika kitu.”[2]

Bi maana baada ya alama ya kutwaharika.

[1] al-Bukhaariy (19).

[2] Abu Daawuud (307).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 28-31
  • Imechapishwa: 12/06/2017