13. Dalili ya kwamba washirikina ambao Mtume aliwapiga vita walikuwa wanakiri Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah II

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Na maneno Yake Allaah (Ta´ala):

قُل لِّمَنِ الْأَرْضُ وَمَن فِيهَا إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ سَيَقُولُونَ لِلَّـهِ ۚ قُلْ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ

“Sema: “Ni ya nani ardhi na wale waliokuwemo humo mkiwa mnajua?” Watasema: “Ni ya Allaah pekee” Sema: “Je, basi kwa nini hamzingatii?”” (23:84)

MAELEZO

Aayah hizi zinafahamisha kuwa washirikina ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitumwa kwao, walikuwa wakithibitisha Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Walikuwa wakithibitisha ya kwamba ardhi na vilivyomo ndani yake ni vya Allaah peke Yake na kwamba hana mshirika. Walikuwa wakithibitisha kuwa Allaah ndiye ambaye ameziumba mbingu na ardhi na kwamba Yeye ndiye Mola wa ´Arshi Tukufu. Walikuwa wakithibitisha kuwa mikononi Mwake ndio kuna wendeshaji wa kila kitu. Walikuwa wakithibitisha kuwa Yeye ndiye Ambaye analinda na halindwi. Haya yote yanawalazimu kumwabudu Yeye peke Yake. Kwa ajili hii ndio maana mwishoni mwa kila Aayah kunakuja makemeo.

Isitoshe zipo Aayah nyingi zinazojulisha kuwa washirikina ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitumwa kwao walikuwa wakithibitisha Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 23/04/2022