13. Kuchunga udugu na matahadharisho ya kukata udugu

27 – ´Aliy bin ´Abdillaah ametuhadithia: Anas bin ´Iyaadhw ametuhadithia: ´Abdullaah bin Yaziyd bin Qusaytw amenihadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Sa´iyd bin al-Musayyab, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Allaah ameumba udugu kama tawi na akasema: ”Je, huridhii Nimwingize Peponi yule anayekuunga na nimwingize Motoni yule anayekukata?”

28 – Abul-Waliyd ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan bin Husayn na Muhammad, ambao wamemsikia az-Zuhriy, kutoka kwa Muhammad bin Jubayr bin Mutw´im, kutoka kwa baba yake, ambaye amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Hatoingia Peponi mkataji.”

29 – Abul-Waliyd ametuhadithia mfano wa hayo: Sufyaan bin ´Uyaynah ametukhabarisha, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Ibn Jubayr, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 125-126
  • Imechapishwa: 05/01/2025