26 – ´Abdullaah bin Yaziyd al-Muqriy’ ametuhadithia: Haywah ametuhadithia: Abu´Uthmaan al-Waliyd bin Abiyl-Waliyd amenihadithia, kutoka kwa ´Abdullaah bin Diynaar, kutoka kwa Ibn ´Umar, kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Hakika wema bora kabisa ni mtu awaunge wale watu ambao baba yake alikuwa akiwapenda.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 124
  • Imechapishwa: 05/01/2025