25 – ´Abdullaah bin Swaalih ametuhadithia: al-Layth amenihadithia: Ibraahiym bin A´yan amenihadithia (´Abdullaah bin Swaalih amesema: “Nimeyasikia haya moja kwa moja kutoka kwa Ibraahiym”), kutoka kwa al-Hakam bin Abaan, kutoka kwa ´Ikrimah, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mzazi akimtazama mtoto wake na akafurahishwa naye, ni kama vile mtoto ameacha mtumwa huru.”[1]

[1] Cheni yake ya wapokezi ni nzuri kwa mujibu wa al-Haythamiy katika “Majma´-uz-Zawaa-id” (8/286)).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 123
  • Imechapishwa: 05/01/2025